top of page

SHEREHE YA KIWANDA CHA BURUDANI NA MDUNDO TANZANIA. 

Tarehe 21 Novemba ilikuwa siku maalumu kwa Mdundo Tanzania pamoja na wadau wa muziki wa Tanzania kwa uwepo wa Tanzania Industry Stakeholders. Lengo kuu likiwa kujadili mustakabali wa soko la muziki Tanzania na namna tunaweza kuzivuka changamoto zilizopo ili wasanii wafaidike na sanaa yao lakini pia kufika anga za kimataifa.

 

Mshereheshaji wa siku Bi. Khalila Mbowe alinogesha shughuli nzima kwa kuhakikisha wahudhuriaji wanashiriki kikamilifu kwenye mijadala lakini pia kuchangamsha kwa maswali yaliyohusiana na muziki wa nyumbani. Mkurugenzi Mtendaji wa Mdundo Tanzania Bi. Maureen Njeri alianaza na kutambulisha timu ya Mdundo ya Tanzania, akaendelea na kueleza historia ya Mdundo Tanzania na muziki unaopatikana Mdundo, pia alidokeza kuwepo ushiriakiano kati ya Mdundo na Foundation ya benki ya CRDB. Ushirikiano huo unategemewa kuleta mageuzi makubwa kwa tasnia ya muziki.

 

Majadiliano kamili yalianza wakati jopo la wataalamu na wadau wa muziki wa Tanzania walipo zungumzia mustakabali wa soko la muziki Tanzania na vitu vya kurekebisha ili muziki wetu kukua zaidi. Jopo liliongozwa na mshereheshaji wa siku Bi. Khalila Mbowe pamoja na Amani Martin ambaye ni Meneja wa Masoko na Ubinifu wa benki ya NMB, Emmanuel Kiondo ambaye ni Mkuu wa Masuala ya Kampuni kutoka CRDB, Fido Mgaigai ambaye ni mtaarishaji, msanii na mtangazaji wa muziki wa Singeli, Benedicto Anthony ambaye ni Mtangazaji na Mkuu wa Idara ya Digitali kutoka Crown Media, Bi. Lucy Tomeka kutoka Mwananchi Communication Limited.

 

Masuala mbalimbali yaliweza kuzungumziwa lakini machache ya muhimu yalitiliwa mkazo ikiwemo suala la wasanii kufikisha jumbe zao kwa kutumia lugha nzuri isiyo na maneno yasiyo sawa, jambo hili lilisitizwa haswa na Bw. Fido Mgaigai mabaye anafanya kazi na wasinii hususani wa singeli kwa ukaribu sana, lengo likiwa kuteka soko la Tanzania na kimataifa.

 

Jambo jingine liliopewa uzito ni umuhimu wa wasanii kujizingatia hususani kwenye suala la kukuza chapa zao (brand) na kuwekeza kwa vitu vya kukuza hadhi zao basi wataweza kupata nafasi wanazostahili kuzipata, suala hili lilitiliwa mkazo na Bw. Benedicto Anthony lakini pia Bw. Amani Martin ambao wote wameweza kufanya kazi kwa ukaribu na wasanii wa muziki. Bw. Kiondo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha alisisitiza umuhimu wa wasanii kupata elimu ya fedha ili kuweza kuepuka kuishiwa pale tu wanapoapata changamoto hususani wakiwa wameshuka kimuziki. Alisisitiza umuhimu wa wasanii kuwekeza kwenye muziki wao kwa kufikiria wakati wa mbele, kwa kuweka bima, kununua hisa na kuwekeza kwenye miradi ambayo itaendelea kuwapa mapato zaidi. Bw. Kiondo alitoa rai kwa taasisi za fedha kuwapa wasanii elimu ya fedha.

 

Uwepo wa tukio hili umeweka nuru mpya kwa tasnia ya muziki Tanzania. Tukio zima lilifana na burudani ilikuwa ya kutosha na wahudhuriaji walipata nafasi ya kusabahiana na kujadiliana masuala muhimu kwaajili ya tasnia ya muziki, na itoshe kusmea yajayo yanafurahisha.


Comments


bottom of page